Enock Maregesi Quotes

Biography

Type: Novelist

Born: in Mwanza, Tanzania

Died:

Enock Maregesi was born in Tanzania. He is the author of "Kolonia Santita", a novel.

Enock Maregesi Quotes

Be nice to the environment. Be nice to animals. Be nice to people. If you do that, you will leave a mark on the world.

Imani ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana na hupeleka watu kwenye ukweli. Kuamini hupotosha, na ni nia ya kudharau kinachoweza kujulikana.

Kama umefanya au umesema kitu kibaya na ukasema ukweli mbele ya mtu au ya watu, omba msamaha kupata tena kibali cha umma.

Tunasema uongo kwa sababu hatuna ujasiri wa kusema ukweli. Ukweli hautupi uhuru, unatupa upweke.

Ukisema ukweli utapata uhuru wa nafsi. Ukisema uongo utapata uhuru wa umma. Heri uhuru wa nafsi kuliko wa umma.

Mungu ni mwingi wa hekima, lakini kwa nini alimuumba Shetani? Kwa sababu, Shetani wakati mwingine ni hekima. Ukiendelea kupigwa, bila wewe kupiga, unaweza kuumia, familia yako inaweza kuumia pia! Kuepusha matatizo ya familia yako, wakati mwingine unahitaji kupigana.

Geuza hasira yako kuwa hekima.

Wengine hatuishi kama wafalme kwa sababu ya nguvu za giza – zilizopo kati ya Mungu na wanadamu. Nyota zetu zimefunikwa. Una kila kitu unachotafuta, ndani ya moyo wako. Usitafute furaha, utajiri au amani nje ya moyo wako. Tafuta furaha, utajiri au amani ndani ya moyo wako.

Kuikaribisha amani ya Mungu katika maisha yangu kumenisaidia. Naishi mbinguni duniani.

Ukitaka kujua maana halisi ya maisha yako kuwa tayari kufanya vitu vikubwa vitakavyohitaji nguvu ya Mungu kuvikamilisha – na kudumu katika maisha hayo kwa kafara ya maombi.

Shetani hataacha kukuandama. Atakuandama mpaka siku utakapookoka. Yaani, siku utakapookolewa na Yesu Kristo, siku ambapo Shetani hatakuwepo tena. Silaha kuu tunayotakiwa kuwa nayo ni imani. Mungu hababaishwi na matatizo yako. Anababaishwa na imani yako.

Unapokumbana na matatizo makubwa katika maisha yako ujue Mungu ana mpango maalumu na maisha yako. Ndiyo maana Shetani anakuandama hivyo.

Unapokuwa na matatizo makubwa katika maisha, Shetani anakuandama sana, Mungu ana mpango maalumu na maisha yako.

Mungu alitengeneza familia. Alitengeneza koo, makabila na mataifa, ili watu wajuane na kuheshimiana.

Tayari Mungu ameshakufadhili. Tafuta kibali chake uishi kama anavyotaka. Kibali cha Mungu ndiyo mtaji wa maisha yako.

Kuvunja sheria ni sawa na kufanya kosa, na kwa hiyo kuwa mkosaji, mbele ya sheria na mbele ya mungu.

Tunapenda kuamini kwa sababu kuamini hurahisisha mambo… Usiamini. Jua.

Kwa sababu ya udadisi wa hali ya juu nasoma kila kitu ninachokutana nacho hasa vile visivyonipendeza. Ukitaka kupata maarifa usisome tu vitabu vinavyokupendeza. Soma vitabu visivyokupendeza.

Nina matatizo ya kiafya: Udadisi wa hali ya juu wa kiakili.

Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu.

Pesa ni ya muhimu kwa sababu ya mahitaji ya lazima ya wanadamu kama vile chakula, maji, malazi, elimu, usafi, mavazi, na afya, lakini ni ya maana kwa sababu ya wanawake.

Jielimishe, usitegemee walimu kukuelimisha.

Tunapaswa kujisikia furaha kuu tunapokumbana na majaribu mbalimbali katika maisha yetu, tukijua kwamba kujaribiwa kwa imani yetu hutufanya wavumilivu na wapiganaji katika Jina la Yesu, na tunapaswa kuruhusu uvumilivu katika maisha yetu kwa sababu Mungu hutumia uvumilivu huo kutukomaza na kutukamilisha.

Maombi yako yasipojibiwa usikate tamaa, Mungu alishakusikia na tayari alishaandaa malaika wa kukuletea jibu. Jibu wakati mwingine huchelewa kufika kwa sababu ya nguvu za giza. Usiwe na haraka, muda wako ukifika utajibiwa.

Lengo la jina la kitabu ni kuishawishi hadhira kusoma dibaji, na lengo la dibaji ni kuishawishi hadhira kusoma salio la kitabu kizima.

Wasifu wa viongozi wa Kolonia Santita ni siri kwa sababu siri ni siri ya mafanikio.

Wakati mwingine tukitaka kufanikiwa lazima tujifunze kutunza siri.

Kutunza siri wakati mwingine ni kitu kigumu sana kwa baadhi ya watu lakini watu wanapaswa kuwa na uwezo wa kutunza siri kujijengea uaminifu, ambao ni siri ya mafanikio.

The biggest barrier in success is the nightmare – You will have to endure the nightmare to be successful.

Ukitaka kutambulika usione aibu.

Wakati ndege inapaa huwa inapambana na upepo. Lakini inapaa, hata hivyo.

Kufanikiwa katika maisha lazima usimamiwe na nguvu za nuru au nguvu za giza. Kama ni nuru lazima ubobee katika nuru. Kama ni giza lazima ubobee katika giza.

Maendeleo ya mtu yatatokana na juhudi za mtu mwenyewe.

Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi.

Serikali mara nyingi hutegemea ujasusi wa ndani na nje kufanya maamuzi mazito na sahihi ya kuendesha nchi.

Hii ni sheria ya akili yangu: Akili yangu ni muhimu kuliko familia yangu. Nisipoitunza vizuri akili yangu, sitaitunza vizuri familia yangu.

Akili yako isipokuwa timamu, familia itakushinda. Familia ikikushinda utalaumiwa na Mwenyezi Mungu.

Maisha tunayoishi ni mafupi, maisha ya mbinguni ni ya milele. Fundisha familia yako upendo na hofu ya Mungu, kwani hiyo ndiyo akili kushinda zote. Hekima ya kutunza familia inapatikana katika kitabu cha Mithali cha Agano la Kale.

Mwaka mpya ukifika watu husherehekea kwa vifijo na nderemo! Pumzi ikifika hawasherehekei. Kwa nini?

Mwanamke akikuomba pesa, mpe!

Mwaka mmoja na nusu unatosha kumjua mwanamke kabla ya ndoa. Miezi sita itakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mchumba. Mwaka mmoja na nusu utakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mke.

Kama unataka kuijua vizuri historia ya mwanamke hasa mwanamke unayetaka kuoana naye, usifanye naye mapenzi kwa miezi sita angalau. Ukifanya naye mapenzi kwa miezi sita au zaidi, au ndani ya miezi sita, halafu akakuchanganya kimapenzi, hutakuwa na uwezo mkubwa wa kuwasikiliza watu kuhusiana na historia yake.

Ukitaka kumjua mwanamke jua historia yake.

Ukikosana na mwanamke usimpige mchana. Mpige usiku. Ukimpiga mchana watu watasema umemwonea. Ukimpiga usiku watu watasema huenda alikuwa na makosa. Wanawake hawatakiwi kupigwa.

Mtu akikutukana mwambie asante au samahani. Asante au samahani vina nguvu kuliko kuomba (asikutukane) au kutukana.

Wananchi wataendelea kuwepo hata kama serikali haitakuwepo. Serikali haiwezi kuwashinda wananchi. Sauti ya umma ni sauti ya Mungu. Serikali haiwezi kumshinda Mungu.

Wananchi wakiamua kufanya kitu katika nchi yao kwa asilimia 100 serikali, na taasisi zake zote, haitaweza kuwazuia. Kwa sababu, mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali.

Serikali imepewa mamlaka na wananchi kuwaendeshea nchi yao. Mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali.

Mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake ana uwezo wa kufanya chochote.

Mtu aliyepoteza kazi na mke na watoto wake kuuwawa kwa mfano, watu wanapaswa kuwa makini na yeye, ana uwezo wa kufanya chochote.

Tumaini lina nguvu kuliko woga… Usisimame. Endelea kutembea.

Kujenga urafiki na wanasiasa wakati mwingine ni kitu kizuri. Wanasaidia kurahisisha mambo.

Kushirikiana na maadui wa nchi yetu ni hatia ya kosa la uhaini. Adhabu yake ni kifo, au kifungo cha maisha.

Kusaliti nchi, ambayo majeshi ya ulinzi na usalama yameundwa kuilinda, ni miongoni mwa makosa makubwa kabisa kuweza kufanywa na mtu! Adhabu yake ni kifungo cha maisha jela, au kunyongwa hadi kufa.

Unaweza kusaliti nchi kwa sababu za kiitikadi, kisiasa, matatizo ya akili, au pesa. Ukifanya hivyo na ukabainika; utawajibika kwa adhabu ya kifo, au maisha.

Serikali inayodhulumu wananchi wake ni hatari kuliko simba.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Tanzania alikuwa mlezi; wa ndoto ya haki, amani, uzalendo, ujamaa, na uhuru.

Kujamiiana si anasa tena katika maisha yangu. Ni hitaji muhimu kwa ujenzi wa familia.

Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa waamini. Wanajijua vizuri zaidi, kuliko unavyowajua.

Mungu alisema tupendane katika shida na raha; Luka 6:27-36. Katika matatizo mpende hasimuyo. Maumivu ya watu hufanana.

Maumivu ya matatizo ya yule aliyekukosea hayana tofauti na maumivu ya matatizo ya wewe uliyekosewa. Adui yako (kwa mfano) akifiwa na mke aliyempenda sana, atajisikia vibaya kama utakavyojisikia vibaya kufiwa na mke uliyempenda sana. Kuwa na huruma kwa waliokukosea, wakati wa shida.

Uko wapi ubinadamu wa watu?

Ikiwa hakuna kitu kinafanyika katika maisha yako usijali. Kuna kitu kinafanyika – kuingia na kutoka kwa hii pumzi.

Kama mwanadamu una haki ya msingi kuwa na amani katika maisha.

Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu.

Iwapo kila mtu atamheshimu mwenzake kama anavyojiheshimu mwenyewe; tunaweza kuishi mbinguni duniani ... lakini kwanza tuwe na maarifa binafsi.

The best prize life has to offer is not a chance to work hard and be something in the community. It is the perfume of God that resides within you.

Usiifundishe familia yako anasa. Ifundishe upendo, unyenyekevu na hofu ya Mungu. Ukiifundisha anasa utahatarisha maisha ya mbinguni ya familia yako, na ya kwako pia.

Nilijitolea sehemu ya maisha yangu ya kijamii na kifamilia kuweza kuchapisha Kolonia Santita katika kiwango nilichokitaka.

Your dreams won’t die until you die don’t ever stop believing!

No matter how talented or skilled you are, you will never reach your full potential without expert guidance.

Hutaweza kufikia malengo yako kikamilifu bila msaada wa wataalamu – Hata kama una kipaji au ujuzi kiasi gani.

Msichana wa miaka 18 miaka ya 70 ni sawa na msichana wa miaka 8 leo. Msichana wa miaka 8 leo anayajua maisha kuliko msichana wa miaka 18 miaka ya 70. Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa.

Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho.

Wape watoto uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa shaghalabaghala.

Nimewapa watoto wangu kila kitu katika maisha isipokuwa umaskini. Lakini bado wamenishinda.

Wape watoto wako urithi wa kutosha ili waweze kufanya kitu, lakini si urithi wa kutosha ili wasiweze kufanya kitu. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata, uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa kila kitu.

Ukiwapa watoto wako uhuru wa shaghalabaghala au uhuru wa kila kitu watajisahau! Wape uhuru wa mahesabu.

Kucheza muziki si lazima utingishe mwili kama mwendawazimu. Unaweza kucheza kwa hisia.

Ukiipenda sana nchi yako ni rahisi sana kuichukia serikali yake!

Kati ya nchi yako na serikali yako ni kitu gani unakipenda zaidi? Ipende zaidi nchi yako, kuliko serikali yako!

Ukitaka kuleta mabadiliko katika dunia huna budi kubadilika wewe kwanza. Ukibadilika ukawa mwema katika jamii yako umeleta mabadiliko katika dunia.

Usuluhishi ni dawa ya uhusiano mwema miongoni mwa watu.

Upendeleo na msamaha ni sumu na baraka ya usuluhishi miongoni mwa watu kwa mpangilio huo. Yaani, upendeleo ni sumu ya usuluhishi, msamaha ni baraka ya usuluhishi. Usuluhishi wenye msamaha, usiokuwa na upendeleo wowote, ni dawa ya uhusiano mwema miongoni mwa watu. Upendeleo ni sumu ya usuluhishi – Msamaha ni kiuasumu cha usuluhishi.

Ukiwapa watu kile wanachokitaka wataendelea kukihitaji.

Silaha kuu ya uchoyo ni kujitolea kwa ajili ya watu wengine. Ni upendo.

Kitabu cha 'Kolonia Santita' ni kitabu cha wasomi na wasiokuwa wasomi, watu wa mijini na watu wa vijijini, watu wazima, vijana na watoto. Hadhira ya kitabu hiki ni jamii nzima ya Tanzania.

Watu hubariki wenzao ambao ni wakarimu, na hulaani wenzao ambao ni wabahili. Ukiwa mkarimu kwa watu umekopa neema kutoka kwa Mungu, na Mungu atakulipa kutokana na matendo yako.

Watu wenye ujuzi au vipaji wanatakiwa kwenda shule kusomea ujuzi au vipaji vyao – kwa miezi mitatu au sita angalau.

Toa msamaha kwa waliokukosea kwa sababu dhambi zilizofanya mkosane zilitoka kwa Shetani.

Maskini mwenye pesa nyingi ni tajiri bahili. Tajiri mwenye mifuko iliyotoboka ni tajiri badhiri.

Falsafa ya Usawa kwa Watu na Vitu Vyote ya Yin-Yang ya Kichina ni falsafa inayotumiwa na Wachina, kujifunza sanaa ya mapigano na kutengeneza madawa ya asili, na magaidi wa madawa ya kulevya wa Amerika ya Kusini na Kaskazini kusaidia watu waliosahauliwa na serikali zao.

Mtu anayesema pesa haijampa furaha hana nia ya kusaidia watu.

Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka.

Toa msaada katika jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo.

Neno moja kutoka mdomoni mwako linaweza kukuletea madhara makubwa. Waweza kusema kitu ukadhani umepatia kumbe umeharibu. Fikiria kwanza maana ya kitu unachosema, halafu sema.

Kuwa mwangalifu unapoongea na watu. Huwajui!

Halafa hailipi.

Nitajisikia raha sana kufungwa kwa ajili ya matatizo watu.

Usiwapoteze marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wako, wala usiwaache marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wao.

Marafiki zako wa mwanzo ni wazuri kuliko wote.

Uwezekano wa watoto wa ukoo mmoja kuoana ni mkubwa kwa sababu damu ina nguvu ya uvutano. Kuhakikisha kwamba familia zinafahamiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ni jukumu la wazazi.

Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa.

Mtu yoyote anayedanganya ni Shetani, kwani Shetani ni baba wa uongo. Tusikubali kudanganywa ovyo, hasa watoto wetu, katika kipindi hiki cha utandawazi na teknolojia.

Mdanganyifu hudanganya wanaopenda kudanganywa.

Mwachie mwanao urithi wa kutosha ili aweze kufanya kitu, lakini si urithi wa kutosha ili asiweze kufanya kitu.

Watu wanahitaji elimu na ajira kuwaepusha na janga la madawa ya kulevya.

Ijapokuwa maombi ya sifa yana nguvu kuliko maombi ya kushukuru, kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba.

Usitukane kamwe. Pigana itakapobidi.

Tumaini ni injini ya imani.

Mbili jumulisha mbili wakati mwingine si sawa na nne. Ni sawa na nne jumulisha moja kwa sababu moja ni nguvu ya ushirikiano.

Shetani na wafuasi wake wako kifungoni sasa hivi kwa sababu dhambi walizotenda hazisameheki. Dhambi ya kumkana Mungu na kumkubali Shetani haisameheki. Kwa maana nyingine, ukimuuzia Shetani roho yako jina lako halitaandikwa katika kitabu cha uzima litaandikwa katika kitabu cha mauti. Ukibidika kuuza roho, usimuuzie Shetani, muuzie Yesu.

Pesa ina maana kwa sababu ya wanawake.

Tumia pesa kibahili, si kibadhiri.

Wanaume hujiua kwa sababu ya fedha. Wanawake hujiua kwa sababu ya mapenzi.

Ili kupambana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya katika jamii ya Tanzania, ni muhimu kutoa elimu kwa Watanzania juu ya madhara yanayoambatana na matumizi ya madawa hayo. Tusipambane na madawa ya kulevya peke yake. Tupambane na elimu ya madawa ya kulevya pia.

Wanaume hupenda nyama kwenye mifupa.

Ikiwa huna pesa na una mke na watoto kwa mfano, mke wako (wanawake walio wengi) hatakuona wa maana kwa sababu ya ustawi wa maisha ya familia yake. Ikiwa una mwanamke asiyekuwa na busara au hekima ya kutosha, au mwanamke ambaye akili zake zimefyatuka kidogo, atakusaliti kutafuta bwana au mtu mwenye maana. Kama huna pesa huna maana kwa mwanamke.

Baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika bustani ya Edeni, kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Kwa hiyo dhambi hutokana na maisha, na maisha hutokana na dhambi.

Ni rahisi kushinda vita ya maisha na kuishi mbinguni duniani. Ni vigumu kushinda vita ya dhambi na kuishi mbinguni paradiso.

Kuna vita za aina mbili zinazopiganwa hapa duniani: vita ya maisha na vita ya dhambi. Unaweza kushinda vita ya maisha (maisha ya raha) lakini ukashindwa vita ya dhambi (maisha ya laana). Kushinda vita ya dhambi ni lazima umkaribishe Mwana wa Mungu Mfalme wa Amani, Yesu Kristo wa Nazareti Aliye Hai, kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

Dunia ni uwanja wa vita wa vita ya dhambi ya vita ya maisha! Kuishi maisha ya kufikirika ni kushinda vita ya maisha ya vita ya dhambi. Vita ya dhambi ya vita ya maisha si vita ya kufikirika! Bila Yesu katika maisha yetu hakuna atakayeishinda.

Acha alama katika dunia baada ya kuondoka.

Radia hakuwa na makosa. Wengi huishi maisha yao bure. Yeye aliishi ya kwake kwa ajili ya watu. Hakuishi tu kama raia wa Tunisia. Aliishi kama raia wa uanadamu, maadili mema na uchapakazi. Watu walimsifu kwa kuwa na kaulimbiu ya 'Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta'.

Kuandika hadithi ni kitu kimoja. Kuweka kanuni za fasihi katika hadithi ni kitu kingine.

Kanuni za fasihi ndiyo msingi wa maandiko yote ya kitaalamu hapa ulimwenguni. Watu hawana budi kuzifuata kanuni hizo kama wanataka kutumia vipaji vyao katika ngazi ya kimataifa.

Ford Bronco ilikuwa sehemu ya upelelezi wa polisi wa Tume ya Dunia, na ilipigwa mnada baada ya upelelezi na kesi kumalizika. Kiasi kikubwa cha pesa iliyopatikana kilikwenda kwa WPD – Idara ya Polisi ya Tume ya Dunia – ili iendelee kuimarisha huduma ya kukomesha biashara haramu ya madawa ya kulevya duniani.

Sentensi ni mkusanyiko wa maneno unaoanza na herufi kubwa na kuisha na alama ya kushangaa, kuuliza, au nukta. Sentensi bora ni fupi, angavu, sahihi, yenye mantiki, na kamilifu.

Kuwa makini na kila kitu unachofanya kwa maana ubongo ni kitu cha ajabu, ubongo una uwezo wa kukupotosha.

Tambua vitu vya muhimu katika maisha yako ijapokuwa unaweza kuacha alama katika dunia bila kujitambua baada ya kuondoka.

Sikujui. Lakini naamini hungependa kuishi maisha yako hapa duniani bila kuacha urithi au kumbukumbu ya aina yoyote katika jamii.

Shindana na wenzako kuwa juu zaidi katika tasnia uliyojichagulia.

Fanya kazi kwa bidii na maarifa!

Tumia kipaji ulichopewa na Mungu.

Hufanani na yoyote katika dunia hii. Unafanana na wewe mwenyewe. Usimdharau mtu, humjui!

Tunazaliwa na kufa. Lakini hatujui tunakotoka. Wala hatujui tunakokwenda. Huenda tunatoka na kwenda katika dunia nyingine, ya ulimwengu mwingine, hivyo kutufanya wageni wa dunia yetu wenyewe. Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta.

Kuzaliwa na kuishi ni mibaraka mikubwa ya Mwenyezi Mungu kuliko yote duniani.

Share Page

Enock Maregesi Wiki

Enock Maregesi At Amazon